emblem

The United Republic of Tanzania

Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology
(CAMARTEC)

News

CAMARTEC experts and Kambi ya Simba village leaders.


Mei 31, 2021 hadi Juni 02, 2021, Timu ya wataalam kutoka Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) walitembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya ya Karatu, Kijiji cha Kambi ya Simba, Kijiji cha Gongali, na Kijiji cha Mang’ola Barazani. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kutafuta taarifa muhimu kwa ajili ya kuanzisha Kitovu cha Teknolojia za Kihandisi (Engineering Technology Hub – ETH) ambacho kitatumika kama majaribio (pilot) ili kupata picha na uzoefu wa uanzishwaji na uendeshaji wake.

Kufuatia picha na uzoefu huo, CAMARTEC imejipanga kuutumia uzoefu huo kuanzisha vitovu vya namna hiyo kwenye Kanda tano (5 ) nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano (5) ijayo. Mtazamo mpana wa CAMARTEC kwa miaka ijayo ni kuweza kuwa na vitovu vya aina hiyo katika kila Kata/Kijiji, kutegemeana na umbali wa kuweza kupata huduma kati ya Kata na Kata au Kijiji na Kijiji.

Pamoja na mambo mengine, lengo kuu la CAMARTEC la kuanzisha Kitovu cha Teknolojia za Kihandisi ni kusogeza huduma na teknolojia zake karibu zaidi na wakulima wa ngazi zote pamoja na wadau wengine.